Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wasitazame namba za Kibu - Edo

Kibu Fgh Simba wasitazame namba za Kibu - Edo

Tue, 7 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Edo Kumwembe amesema kuwa Klabu ya Simba wasitazame takwimu za mabao za mshambuliaji wao, Kibu Denis ili kumpa mkataba mpya.

Inaelezwa kuwa Kibu ambaye ana bao moja na mkataba wake unaelekea mwishoni, ameomba mkwanja mrefu ili asaini Simba vinginevyo atasepa.

“Takwimu zinatuonyesha Kevin De Bruyne ni bora kuliko Zinedine Zidane. Macho yetu yanatuambia Zidane ni bora kwa mbali kuliko staa huyu wa Manchester City na timu ya taifa ya Ubelgiji.

“Takwimu zinatuonyesha Cristiano Ronaldo ni bora kuliko Diego Maradona na Ronaldo De Lima. Hali halisi inatuambia hao wawili ni bora kuliko Ronaldo. Hapa ndipo linapoibuka suala la Kibu.

“Hana mabao mengi lakini kuna kitu ambacho Simba wanakiona kwa Kibu kuliko kwa wachezaji wengine. Ukiwaambia Simba nani aondoke kati ya Kibu au Freddy Michael watakwambia Freddy aondoke ingawa ni huyu huyu amefunga mabao mengi kuliko Kibu.

“Soka la namba linatuchanganya katika dunia ya kisasa. Unajaribu kushindana na hali halisi. Hapa ndipo Kibu anapohitaji pesa nyingi katika mkataba wake. Hapo ndipo Kibu anadengua,” amesema Edo Kumwembe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live