Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wasimuache Mangungu atawafikisha kwenye nchi ya ahadi - Eng. Hersi

Hersi Mangungu Pic Data Mangungu na Eng. Hersi.

Thu, 22 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Yanga SC, Eng. Hersi Said amesema kuwa wanachama wa Klabu ya Simba walifanya uamuzi sahihi wa kumchagua Murtaza Mangungu kuwa mwenyekiti wao.

Kupitia kipindi cha Jana na Leo cha Wasafi Media, Eng. Hersi Said amesema; “Wanachama wa Simba wamemchagua Mangungu kuwa Mwenyekiti wa klabu na mimi naheshimu hayo maamuzi.

"Mimi niwaombe Simba wasije wakamuacha Murtaza Mangungu, ni kiongozi mzuri sana na ninaamini atawafikisha Simba kwenye nchi ya ahadi, kama ambavyo amefanya kwenye hii misimu mitatu iliyopita amefanya vizuri sana,” amesema Eng. Hersi Said.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live