Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wasijidanganye wanaweza kushindana na Yanga - Mchambuzi

CHAMA DEBORA MS Simba wasijidanganye wanaweza kushindana na Yanga - Mchambuzi

Wed, 10 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Alex Ngereza amesema kuwa Klabu ya Simba waache kujidanganya kuwa wana uwezo wa kushindana na watani zao wa jadi, Yanga Sc.

"Simba wasije wakajidanganya kwamba wanaweza kushindana na Yanga msimu huu, Yanga wameweza kuwabakisha wachezaji wao wote muhimu na wamesajili wachezaji ambao walikuwa muhimu kwenye timu walizotoka ambazo ni za hapa hapa kwenye ligi yetu",

"Yanga hawatokuwa na kazi kubwa kwasababu kubwa ya wachezaji wao wote tayari wapo kwenye mfumo na hata hawa wachezaji wapya wanaijua ligi vizuri.

"Kwa upande wa Simba wao Wana kazi kubwa ya kufanya kwasababu Kila kitu ni kipya,wachezaji ni wapya na kocha mpya ambapo Wana kazi ya kufanya kuifahamu ligi," amesema Alex Ngereza.

Wanasimba mnasemaje hapa?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live