Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba washusha straika mwingine, wafunga usajili

Simba Mohammed Mussa Simba washusha straika mwingine, wafunga usajili

Mon, 16 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wekundu wa Msimbazi Simba SC, wametangaza kumsajili mshambuliaji mpya, Mohamed Mussa kutoka Malindi ya Visiwani Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa waliyoposti kwenye Simba App, Mussa ambaye mbali na kucheza kama mshambuliaji pia anamudu kucheza kama kiungo wa nafasi zote za pembeni, amesaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia Simba SC.

Taarifa hiyo imeeleza, miongoni mwa sifa zilizowavutia Simba kumsajili mshambuliaji huyo ni kipaji chake halisi cha mpira pamoja na umri wake wa miaka 22 ambao wanaamini atakuwa msaada baadaye.

Taarifa imeeleza, licha ya nyota huyo kutokea visiwani Zanzibar, haitakuwa mara ya kwanza kwake kucheza Ligi Kuu kwani amewahi kuzitumikia Gwambina FC na Mbeya City.

Usajili huo unakuwa ni wa nne kwa Wekundu hao wa Msimbazi katika dirisha dogo lililofungwa Januari 15, 2022, baada ya kusajiliwa Saido Ntibanzokiza, Hamed Sawadogo, na mshambuliaji Jean Baleke.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live