Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba washusha dozi nzito kwa Mtibwa Sugar, Sakho kawa mtamu

Mzamiru Goal.jpeg Simba imeibuka na ushindi wa magoli 5-0

Sun, 30 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wekundu wa Msimbazi, Simba SC wameibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na viungo, Mzawa Muzamil Yassin dakika ya 38, Msenegal Pape Ousmane Sakho mawili dakika ya 48 na 90 na ushei na mshambuliaji Mzambia, Moses Phiri mawili pia, dakika ya 63 na 73.

Mtibwa Sugar walijikuta wakimaliza mchezo wakiwa pungufu baada ya wachezaji wao wawili Pascal Kitenge na Cassian Ponera kuoneshwa kadi nyekundu.

Kwa ushindi huo, Simba SC wanafikisha pointi 17 na kupanda nafasi ya pili, sasa wakizidiwa pointi tatu na mabingwa watetezi, Yanga SC baada ya wote kucheza mechi nane, wakati Mtibwa Sugar inayobaki na pointi zake 15 za mechi 10 wanashukia nafasi ya nne.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live