Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba washusha Kocha mpya

DDFF1904 2FDC 48E1 84E3 8A316879FF87.jpeg Kocha mpya wa makipa Simba Queens, Adam Meja

Tue, 11 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabosi wa Simba wamefanya maboresho katika benchi la ufundi la timu ya wanawake, Simba Queens, kwa kumleta kocha wa makipa, Adam Meja kutokea Dodoma Jiji iliyopo Ligi Kuu Bara.

Inaelezwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ kabla ya kutua Angola kushuhudia mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Primeiro de Agosto alikuwa amekamilisha dili hilo.

Simba imemleta ili kuongezea nguvu benchi hilo na kuwanoa pamoja na kuongeza ubora wa makipa wanne wa Simba Queens, Gelwa Yona, Caroline Lufa, Zubeda Mgunda na Janeth Shija.

Inaelezwa Meja atapewa nafasi ya kwenda kufanya mazoezi na kuwanoa makipa wa timu ya wanaume, Aishi Manula, Benno Kakolanya na Ally Salim kama ikitokea dharura yoyote.

Uamuzi wa kumleta Meja na kupewa muda wa kufanya kazi na kina Manula, ni ushauri wa kocha mkuu, Juma Mgunda kisha uongozi ukalitekeleza.

Hii ni mara ya pili kwa Meja kurejea Simba aliwahi kufanya kazi ya kuwanoa makipa enzi za kocha Jackson Mayanja “Mia Mia’.

Simba Queens inajiandaa na fainali za Klabu Bingwa Afrika zinazofanyika Morocco kati ya Oktoba 30 - Novemba 13.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live