Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba washauriwa kutobweteka

F83bf39639f8f7d5231c354354b585f3 Simba washauriwa kutobweteka

Wed, 2 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MSHAURI wa Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, Crescentius Magori amewataka wekundu hao wa Msimbazi kutobweteka na ushindi wa bao 1-0 waliopata dhidi ya Plateau United ugenini Nigeria bali kujipanga kumaliza kazi salama.

Wawakilishi hao wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika walianza vyema katika mchezo wa kwanza dhidi ya timu hiyo ya Nigeria kwa ushindi wa bao 1-0 na Jumamosi ya wiki hii watarudiana ili apatikane mshindi atakayesonga mbele hatua inayofuata.

Akizungumzia mchezo huo, Magori alisema wapinzani wao wanaweza kuja na kasi ya kutaka kulipiza kisasi hivyo ni muhimu kujipanga na kutojisahau.

“Wachezaji wamefanya kazi kubwa kwa kujituma ugenini na kupata ushindi sasa tusibweteke wanaweza kuja kivingine ili kujaribu kufanya vizuri Dar es Salaam,” alisema.

Alisema ana amini kwa uwezo wa timu yao wanaweza kufanya vizuri na kufuzu hatua inayofuata.

Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo Barbara Gonzalez ameomba wapenzi na wadau wao kuiombea timu ili ifanye vizuri.

“Tunaomba wapenzi wetu kule nyumbani watuombee dua ili Jumamosi tumalize kazi na kukutana na FC Platnum, ukimtanguliza Mungu siku zote unapata ushindi,” alisema.

Kikosi cha Simba kiliwasili jana jioni kujiandaa na mchezo huo wa marudiano utakaochezwa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Iwapo Simba itashinda na kuvuka hatua hiyo ya awali, bado watakuwa na kibarua kingine cha kukutana na kati ya FC Platnum ya Zimbabwe au Coasta Do Sol ya Msumbuji.

Katika mchezo wa kwanza Platnum walishinda mabao 2-1 ugenini.

Chanzo: habarileo.co.tz