Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba warejea nchini, kituo kinachofuata ni Kagera Sugar

Simba Warejea Nchini, Kituo Kinachofuata Ni Kagera Sugar Simba warejea nchini, kituo kinachofuata ni Kagera Sugar

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba SC wametua nchini wakitokea nchini Morocco walipokuwa wamekwenda kukipiga na Wydad AC na kupokea kichapo cha 1-0.

Simba watajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC utakaopigwa Ijumaa hii Desemba 15, 2023 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar dhidi ya Kagera Sugar.

Akimalizana na Kagera, Simba atarejea tena Klabu Bingwa kuindaa kucheza tena na Wydad mchezo nne wa Makundi katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.

Kwenye kundi B, Simba wanashika mkia wakiwa na alama 2 huku vinara wakiwa na ASEC Mimosas wenye alama 7 wakifuatiwa na Jwaneng wenye alama 4 na Wydad akiwa na alama 3.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live