Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wapo tayari asilimia 100 kwa Msimu mpya

SIMBA TRAINING Kikosi cha Simba kikiendelea na Mazoezi Jijini Arusha walipoweka Kambi

Tue, 7 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ndivyo unavyoweza kusema baada ya kikosi cha Simba SC kuendelea na mazoezi kule Mkoani Arusha walipoweka kambi kwa mara ya pili wakijiandaa na Msimu mpya wa Ligi na ule wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizingumzia kwa ujumla ubora wa maandalizi yao Mratibu wa kikosi hicho Abbasi Ally amesema;

"Kinachoendelea kwa sasa ni mazoezi ya kawaida ya timu kama timu nyingine ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi , na tunafanya mazoezi mara mbili kwa siku"

"Wachezaji tulionao hapa ni ishirini na tatu (23) na hakuna mchezaji wetu yeyote ambae anakosekana zaidi ya wale walioitwa timu zao za taifa tu" amesema Abbas

Simba haijaweka wazi kama aidha katika maandalizi ya kambi yake Jijini Arusha itacheza mechi za kirafiki ama la japokua kuna tetesi kuwa itacheza na Namungo ambao nao wameweka kambi kule Karatu.

Simba pia itacheza mchezo wa Kimataifa wa kirafiki na Klabu ya kutoka DR Congo, TP Mazembe katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya Simba Day Septemba 19.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live