Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wapo kimya kama hawapo vile

Mashabiki Simba Kwa Mkapa.jpeg Simba wapo kimya kama hawapo vile

Thu, 18 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati mechi ya watani wa jadi inakaribia, kikosi cha Simba SC kinaendelea kujifua mjini Zanzibar, huku silaha ya viongozi wa timu hiyo kwa sasa ikiwa ni kuwa kimya, lakini wakiwa kwenye mikakati mikali ili kuhakikisha inashinda.

Habari kutoka ndani ya klabu hiyo, zinasema kuwa viongozi wa klabu wanaelewa kila kitu kinachoendelea kwa waandishi wa habari, wachambuzi na hata mashabiki wa soka wanaipa nafasi kubwa Young Africans, huku wakiibeza timu yao, na hilo limewapa nafasi ya kukaa kimya bila kuongea neno lolote, lakini wakiwa kwenye mikakati mbalimbali kuhakikisha wanashinda mechi hiyo na kujiongezea pointi tatu.

"Mikakati inayofanywa ni kuzuia hila na mbinu zozote chafu ambazo zinaweza kutumika ili kupoteza mechi, kwa sababu wanaamini hata mechi iliyopita hawakufungwa mabao 5-1 kwa kuzidiwa sana na watani zao, ila kuna mbinu ambazo walizigundua mara tu baada ya mechi," amesema mtoa habari.

Amesema moja ya mikakati hiyo ni kuiondoa timu Dar es salaam na kuipeleka, Zanzibar, hivyo kubainisha kuwa mechi ya Jumamosi haitokuwa rahisi kwa Young Africans kama wengi wanavyodhani.

"Mechi ile kuna baadhi ya wachezaji waliondoka kambini, hawakulala kambini kuelekea siku ya mechi, wakarejea asubuhi, lakini cha kustaajabisha, pamoja na baadhi ya wadau wa karibu kutaka wasichezeshwe kwa sababu wamekiuka miiko ya kambi.

"Lakini walicheza na kile ndicho kilichotokea, safari hii kitu cha kwanza ni kuwaondoa mjini kwanza, mengine wanaendelea kuyafanyia kazi, kwa hiyo nakuhakikishia viongozi na wadau wengine walioletwa kuongeza nguvu wapo mzigoni, mechi haitokuwa ya kitoto kama watu wanavyodhani, tahadhari zote zimechukuliwa," kilisema chanzo hicho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live