Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wapigwa bao 5, Maxi ampelekea moto Manula

Simba Vs Yanga Aziz Ki Debut.jpeg FT: Simba 1-5 Yanga

Sun, 5 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Timu ya Yanga wametoa kipigo kizito kwa watani zao wa Jadi Timu ya Simba SC mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo Novemba 5 katika Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo ambao Simba ndio waliokuwa wenyeji, Yanga walianza kwa kasi tangu kipindi cha kwanza na kujipatia bao la mapema kutoka kwa mahambuliaji wake Kennedy Musonda dakika ya 3.

Kibu Denis aliwarudisha Wekundu wa Msimbazi katika mchezo baada ya kusawazisha bao dakika ya 9 ya mchezo na kufanya matokeo kuwa 1-1 mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika.

Kipindi cha pili Yanga walirudi kwa kasi na mbinu mpya na kujipatia mabao kupitia kwa Maxi Mpia nzengeli aliefunga mabao mawili, Stephen Aziz KI na Pacome zouzoua aliefunga kwa mkwaju w penati.

Mpaka dakika 90 zinakamilika Yanga wameibuka ma ushindi wa magoli 5-1 na kupaa mpaka kileleni mwa msimamo wa Ligi wakifikisha alama 21 Azam nafasi ya pili na alama zake 19 huku simba wakibaki nafasi ya tatu na alama zao 18 na mchezo mmoja mkononi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: