Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wapiga tizi la mwisho nchini tayari kuwafata Wydad

Simba Tizi La Mwisho Dar Simba wapiga tizi la mwisho nchini tayari kuwafata Wydad

Tue, 5 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wekundu wa Msimbazi Simba SC leo Desemba 5, 2023 wamepiga tizi la mwisho asabuhi tayari kabisa kujiandaa na safari ya nchini Morocco kuwafata Wydad Casablanca.

Kupitia ukurasa wao wa Instagram, Simba wameposti picha za mazoezi na kuainisha kuwa ndio ya mwisho kabla ya kuwafata Wydad.

Simba watacheza mchezo huo muhimu kwao Jumamosi hii Desemba 9, 2023 ambapo Wydad nao wanautaka mchezo huo wa nyumbani ili kuwa wa kwanza kupata matokeo baada ya kupoteza muchezo yote miwili ya awali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live