Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wapewa somo namna ya kujenga timu tishio

Partick Phiri Simba Patrick Phiri

Sat, 11 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Simba jioni ya leo kinatarajiwa kushuka Uwanja wa Manungu, Turiani kuvaana na Mtibwa Sugar katika pambano la Ligi Kuu Bara, ikiwa ni siku chache tangu itoke kufanya kweli kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuifunga Vipers ya Uganda kwa bao 1-0.

Simba inashika nafasi ya pili kwenye msimamo ikikusanya pointi 54, kupitia mechi 23, ikiwa nyuma ya vinara Yanga yenye pointi 62 kwa idadi kama hiyo ya mechi, lakini kocha wa zamani wa timu hiyo, Patrick Phiri amesema amekiangalia kikosi hicho cha Msimbazi na kubaini kuna tatizo.

Mzambia huyo aliyeipa Simba ubingwa bila kupoteza mechi 2009-2010 amesema Simba ya sasa sio kama ilivyozeleka kwa miaka misimu minne iliyopita na inapaswa kurekebisha hasa safau ya ushambuliaji kwa kutafuta mchana nyavu atakayewapa raha Wanasimba.

Phiri aliyewahi kuinoa timu hiyo kwa awamu tatu tofauti na mara ya mwisho ikiwa msimu wa 2014-2015, aliliambia Mwanaspoti kuwa, viongozi wa Simba kwa kushirikiana na benchi la ufundi wanapaswa kufanya kitu ambacho kitawasaidia msimu ujao hasa kwenye eneo hilo la mbele.

Alisema, amekuwa akiifuatilia Simba kila inapocheza, lakini siku za hivi karibuni haridhishwi na kasi ya ufungaji mabao hasa safu ya ushambuliaji na kuwashauri kuwa wanapaswa kusajili washambuliaji halisi. Hata hivyo, Simba ya msimu huu ndio inayoongoza kwa kufunga mabao mengi ikiwa na 55, ila mechi yao yakichangiwa zaidi na viungo washambuliaji, huku mabeki nao wakiwa hawapo nyuma.

Phiri alisema kiuhalisia Moses Phiri aliye kinara wa mabao wa timu hiyo kwa sasa akifunga 10 sawa na Saido Ntibazonkiza sio washambuliaji halisi, lakini wanafanyakazi kubwa ya kufunga.

"Tunachoshukuru Simba wanapata pointi tatu kwenye mechi zao, lakini ukiangalia kiwango chao hakipo katika ubora ule wa Simba ninayoifahamu miaka kadhaa iliyopita ilipotwaa ubingwa mara nne mfululizo," alisema Phiri na kuongeza;

"Hivi sasa wamechelewa na hakuna namna ya kusajili tena, ila wajipange msimu ujao kutafuta mastraika halisia ambao watakuwa na uwezo wa kufunga mara tu wanapopata nafasi za kufunga maana kwasasa kuna tatizo hilo, hakuna wamaliziaji, kila mchezaji anataka kucheza, apige chenga mwisho mipira inapotea."

Phiri ambaye hana timu kwa sasa, alidokeza Simba ina wachezaji kutoka Zambia na sio mara ya kwanza na kwamba wana mchango mkubwa;

"Waanze kufanya skautingi sasa hivi ili usajili utakapofunguliwa waje kumalizia tu, hata wakirudi Zambia wapo wengi na wapambanaji, naamini hawajachelewa," alisema Phiri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live