Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba waonywa mashambulizi kwa Robertinho, watakiwa kusubiri maajabu yake

Robertinho X Ushindi Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira 'Robertinho'

Fri, 24 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa zamani wa Kagera Sugar na Biashara United, Francis Baraza amesema licha ya Simba kupoteza michezo miwili ya Ligi ya Mabingwa Afrika, uongozi na mashabiki wa timu hiyo wanapaswa kumwamini Kocha, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ raia wa Brazil.

Simba imecheza mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika Kundi C na kupoteza zote ikichapwa 1-0 ugenini dhidi ya Horoya ya Guinea na kufungwa 3-0 nyumbani na Raja Casablanca ya Morocco hivyo kuburuza mkia kwenye kundi hilo ikiwa haina pointi.

Mchezo unaofuata Simba itavaana na Vipers ya Uganda Februari 25 ambapo inatakiwa kushinda ili kufufa matumaini ya kufanya vizuri kwenye michezo minne iliyobaki na kutinga robo fainali.

Akizungumza kwa simu kutoka nchini Kenya, Baraza alisema licha ya Simba na Yanga kuanza vibaya lakini kwa hatua zilipofikia (makundi) zimefanya kazi kubwa na aliwapongeza viongozi na wachezaji na kuwataka mashabiki wasibeze juhudi hizo.

Baraza ambaye ni kocha wa Polisi ya Kenya alisema Simba ina uwezo mkubwa wa kumaliza katika nafasi ya pili kwenye kundi lake na kwenda robo fainali huku akiuomba uongozi kumpa sapoti Mbrazil, Robertinho.

“Nikizungumzia kiufundi kwa upande wa Simba kitu kimoja ni kumwamini kocha pamoja na timu yake kwa ujumla na kumpa sapoti yote maana bado kuna chance (nafasi) kubwa ya kusonga mbele, bado kundi lao liko wazi endapo itashinda mechi ya Vipers ya Uganda,”

“Simba ninavyo itambua ina uwezo mkubwa wa kumaliza katika nafasi ya pili ikiwa itaweka kando mechi zilizopita na kuangalia mechi zilizosalia. Nawashukuru viongozi wa Simba na Yanga kwa kufanya kila juhudi kuhakikisha timu timu zao zinafika hatua ya makundi, siyo kazi rahisi kama watu wanavyo fikiria,” alisema Baraza na kuongeza:

“Kwa upande wa Yanga wasibweteke na matokeo dhidi ya TP Mazembe na kama itaweza kucheza vile ilivyocheza kama team, area zote ilicheza kwa kujiamini nidhamu ya hali ya juu na kutumia few chances walizo zipata inawapa nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwa mechi zilizo salia,”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live