Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wanatafuta sababu ya kuachana na Chama - Mchambuzi

Realclatouschama Clatous Chama

Fri, 22 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka Clouds Media, Master Tindwa amedai kuwa uongozi wa Kkabu ya Simba unatafuta njia mbadala ya kuachana na kiunho wake raia wa Zambia, Clatous Chota Chama baada kiwango chake kuporomoka.

Kauli hiyo ya Tindwa inakuja kufuatia taarifa iliyotolewa na uongozi wa timu hiyo jana kuwa Chama na Nassoro Kapama wamesimamishwa kutokana na sababu za utovu wa nidhamu.

“Simba wanatafuta jinsi gani ya kumalizana na Chama , siku hizi Chama amepunguza uzalishaji klabuni lakini amekuwa na sintofahamu nyingi na Klabu”

“Mgogoro wa Chama na Simba haujaanza hivi sasa na kila mmoja kwa nafasi yake anaonekana yupo sahihi na Simba wanaonekana wanatafuta timing tu ya kuachana na Chama.

“Ndio maana kuna mechi Chama hakuanza lakini hakuna anayeuliza kwanini Chama hajaanza,” amesema Master Tindwa.

Chama ambaye alisajiliwa na Simba mwaka 2018 ameisaidia timu hiyo kuchukua Kimbe la Ligi Kuu Bara mara nne mfululizo, Kombe la Shirikisho Tanzania na kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya CAFCL na CAFCC kwa nyakati tofauti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live