Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wanatafuta namna ya kumalizana na Chama

Chama Alamba Dili La Ubalozi Clatous Chota Chama.

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi nguli wa masuala ya soka nchini, Master Tindwa amesema kuwa Klabu ya Simba inatafuta njia nzuri ya kumalizana na nyota wake, Clatous Chota Chama baada ya kuonekana kiwango chake kushuka.

Chama (32) raia wa Zambia ambaye amefanya makubwa kwenye Ligi ya Tanzania, ameringia kwenye mgogoro na timu yake hiyo kwa kile kilichoelezwa kuwa ni utovu wa nidhamu.

“Simba wanatafuta jinsi gani ya kumalizana na Chama , siku hizi Chama amepunguza uzalishaji klabuni lakini amekuwa na sintofahamu nyingi na Klabu”

“Mgogoro wa Chama na Simba haujaanza hivi sasa na kila mmoja kwa nafasi yake anaonekana yupo sahihi na Simba wanaonekana wanatafuta timing tu ya kuachana na Chama”

“Ndio maana kuna mechi Chama hakuanza lakini hakuna anayeuliza kwanini Chama hajaanza,” amesema Master Tindwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live