Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wanasubiri nini kutoa 'Thank You' ya Chama

Chama Ss Simba wanasubiri nini kutoa 'Thank You' ya Chama

Wed, 3 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwisho wa siku Mnyama akija Kutoa hiyo THANK YOU ya Clatous Chama itaonekana kama ametoa taraka kwa shingo upande, jambo halilikuwa na ulazima wowote kusubiria.

Clatous Chama alitakiwa Kupewa THANK YOU siku ambayo Mkataba wake ulimalizika Rasmi. Na hii yote inaletwa na ukweli kwamba hakukuwa na Maamuzi ya pamoja kwenye bodi kuhusu Kuondoka kwa Clatous Chama.

Wengine waliona utumishi wake ndani ya Simba Sports unapaswa kukomea misimu sita na hana Cha kuchangia tena. Wengine walikuwa na Mentality zile zile za Kizamani "Tutamuimarisha Mpinzani".

Ambao walikuwa wanataka abaki ni wachache Lakini Wenye Nguvu sana kuliko wale Wengi ambao walikuwa wanataka aondoke.

Hizi "Indecisions" Simba Sports wanatakiwa kuzirekebisha haraka iwezekanavyo lasivyo Watajikuta wanaanza Ligi wakiwa tayari nje ya Malengo ya Msimu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live