Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wanamtaka Marouf Tchakei

Marouf Tchakei Tizi Marouf Tchakei

Thu, 16 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kumkosa katika dirisha dogo la usajili lililofungwa Januari 2024, mwaka huu, Klabu ya Simba imeanza tena mchakato wa kusaka huduma ya winga na kiungo mshambuliaji wa Ihefu, raia wa Togo, Marouf Tchakei.

Simba SC imepania kwa kiasi kikubwa kufumua kikosi chake na kutengeneza timu mpya yenye ushindani kwa ajili ya msimu jao wa mashindano, inapiga hodi kwa kiungo huyo ambaye anacheza namba moja na Clatous Chama.

Habari kutoka ndani ya Simba SC zinasema huenda safari hii wanaweza nyota huyo kirahisi kutokana na kilichoelezwa pia nyota huyo yuko tayari kupata changamoto mpya lakini bado anabanwa na mkataba wake.

Chanzo kingine kutoka Ihefu kimesema bado ana mkataba, hivyo kama Simba SC inamhitaji italazimika kufanya mazungumzo.

"Tulimhitaji dirisha dogo la usajili, lakini ilishindikana, klabu yake iliweka ngumu lakini mwenyewe alikuwa radhi kujiunga na timu yetu, akatuambia tusubiri msimu uishe atakuwa huru, sisi tunasimamia pale pale, lakini kama itakuwa vinginevyo basi tutaangalia itakavyokuwa lakini ni lazima tumng'oe, tumejidhihirisha ni mchezaji mzuri na atatusaidia sana, ameshaifahamu Ligi ya Tanzania na ameizoea," amesema mtoa taarifa hizi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live