Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wanaendelea kutibu UTI sugu kwa Panado badala ya Azuma

Simba Squad Warm Up.jpeg Simba wanaendelea kutibu UTI sugu kwa Panado badala ya Azuma

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Haya niliyaandika kabla Gigy Money hajachafua Hali ya Hewa… ilikuwa ni 2021 wakati Simba wanamuajiri Pablo kama Kocha wao. Walimpa kila aina ya Utikufu kuwa ni Mwarobaini wa Gonjwa linalowasumbua Simba. Matokeo mnayoyapata sasa ni matokeo ya ujinga mwingi unaofanywa na Viongozi wa Simba toka 2020.

Tukumbushane wakati Pablo anaajiriwa

Kuna Porojo zinaendelea mtaani kuhusu huyu Kocha Mpya wa Simba. Mashabiki wa Simba wote wanaona huu ndio mwarobaini wa Timu yao kufanya vizuri. Leo niwaambie kitu kwenye Soka priority ya kwanza ni Kuwa na Wachezaji ambao ni top players au Wachezaji walio talented au Kwa kifupi kwenye team kunahitajika kwanza Wachezaji Wazuri kabla ya kocha mzuri.

Nina uhakika hata Leo Yanga ikimuajiri Gurdiola Cha kwanza Gurdiola ataomba fungu la kusajili kwanza Wachezaji anaowaamini wanaweza kumsaidia kushinda. Ndio maana kila baada ya Msimu makocha huziambia management zao kuwa wanahitaji kusajili na wanataja kabisa Mchezaji anayemtaka.

Tafsiri yake ni kuwa Coach ana mchango Kidogo Sana kwenye kusaidia team kushinda ukilinganisha na squard aliyonayo hasa Ubora wa Mchezaji mmoja mmoja.

1992 U.S.A ilichagua best players kwenye NBA kuunda Timu yao ya Basketball iliyokwenda kushiriki mashindano ya Olympic. Team hii iliitwa Dream team na ilitoa kipigo Cha kufa mtu kwenye mashindano Yale. Makocha wengi walipohojiwa walisema hii Timu hata kwenye benchi lao la ufundi wakikaa nyani watashinda.

De Rosa aliyefukuzwa Simba kilichombeba kilikuwa ni quality ya Wachezaji aliokuwa nao Haswa Chama na Mickson kwa kipindi kile ndio maana kwenye Match ambazo Chama au Mickson hawakuanza Simba haikushinda Hadi wamuingize aidha Chama au Mickson wakati huo wakiwa kwenye ubora wa hali ya juu. Hii ilikuwa ni chemistry ya Ushindi ndio maana Kocha Sven alikuwa akishinda na aliondoka Simba ikiwa inashinda na De Rosa Naye akarithi kushinda. Chama na Mickson wangelibaki Simba hata matola angelikuwa Head coach asilimia za kuendelea kushinda kila game zingekuwa zaidi ya 95. Matokeo yake wakawauza bila kufikiri mbadala kwa kipindi kile. Wameenda walikoenda na maisha ya Soka yanahitaji Pumzi, Mickson na Chama akili inajua mpira lakin Pumzi ya Yao Yao inawazuia wasimfikie Diara haya ni maisha ya Soka…. Kuna saa akili inataka Mwili unakataa ndio dhana za hujuma huanza kuzungumzwa.

Wakati Pablo anaajirwa niliwaambia ni Kocha wa kawaida Sana, anatokea nchi ambayo ligi yao kwenye ranking za Soka ni ya 145 huku Tanzania ikiwa ni ya 130. Kocha huyu anakuja kukutana na kikosi cha kawaida pia na atahitaji Muda kujaribu kutengeneza Muunganiko Kwa Kutumia Wachezaji waliopo kama itashindikana kabisa kwenye Dirisha Dogo la Usajili lazima Simba waingie Tena sokoni Kwa Haraka Sana ili kuendelea kubaki na Ubora waliokuwa nao.

Kocha aliyefukuzwa Simba ni yule yule ambaye kila Tumi kwenye champions league ikitua Kwa Mkapa inapigwa lakini Juzi walishindwa kabisa kuwazuia Galaxy Timu ya kawaida kabisa ukilinganisha na vigogo wa Soka waliokula kichapo Kwa Mkapa. Issue hapa haikuwa De Rosa au Sven Bali issue hapa ilikuwa quality ya Kina Chama na Mickson na naamini Hawa kina Galaxy wangekutana na kina Chama na Mickson wangetolewa.

Tatizo hili liliwahi kuwapata pia Simba kipindi Mafisango alipopata ajali akafariki. Simba iliyumba Sana, tatizo la Simba wengi hawataki kuamini kuwa mbadala wa Chama na Mickson waliokuwa kwenye ubora bado haujapatikana.

Leo Ukimuweka Mwambusi kwenye Benchi la ufundi la Man City Kwa Aina ile ya Wachezaji ataendelea kushinda as long as anaweza kunyoa kipara kama Gurdiola ????????????????????.

Ni mara chache Sana hutokea Kocha akaleta mabadiliko makubwa kwenye Timu Kwa Kutumia Wachezaji ambao ni average players. Ndio maana hata Makocha wenyewe wanasema Manchester United in 1994 hawakuhitaji Kocha Bora kuwa na Ubora ule as long as ndani ya dimba walikuwepo kina Eric Cantona. Au Maradona hakuhitaji Kocha Bora Sana kuwa Katika kiwango alichokuwepo Hadi anastaafu.

Bado Simba imeendea kununua Panado za kutuliza maumivu badala ya kumenza Antibiotic zijazotibu Ugonjwa uliobainika Maabara baada ya Vipimo.

Huyu Kocha mnataka aje mfundishe Bocco mbinu gani Mpya? Saidoo mnataka afundishwe nini tena? Wachezaji zaidi ya asilimia 90 pale Simba Grisi imeisha kwenye Magoti ni wa kubadilisha.

Kila mashabiki wakipiga kelele wanafukuza kocha na kusema watamsajili mchazaji flan toka Yanga. Kwa sasa wanasema Max yupo kwa Mkopo Yanga wataenda kumsajili na mashabiki kama mazuzu vile wanajichekesha tu.

Share kwa faida ya Makolo. Na Thadei Ole Mushi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live