Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wana nafasi ya kutoboa Makundi Kombe la Shirikisho?

FOTneqiWQAEYAxY Kiungo wa Simba Jonas Mkude, akimiliki mpira mbele ya wachezaji wa ASEC

Mon, 21 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wekundu wa Msimbazi Simba imepokea kichapo cha mabao 3-0 ugenini dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast usiku wa Jumapili ya Machi 20, 2022 kwenye mchezo wa mzunguko wa tano kombe la Shirikisho barani Afrika.

Kwenye mchezo uliochezwa kwenye dimba la Generali Mathieu Karekou uliopo mjini Kotonou nchini Benin, mlinda mlango wa Simba SC, Aishi Manula aliokoa penalti mbili zilizopigwa na Karim Konate na Kouassi Attohoula Yao.

Baada ya kipigo hicho, ASEC Mimosas inashika usukani wa kundi D ikiwa na alama 9, RS Berkane wa pili akiwa na alama 7 sawa na Simba SC inayoshika nafasi ya tatu huku US Gendarmerie akishika mkia akiwa na aalama 5.

Ili Simba SC ifuzu hatua inayofuata ya Robo fainali basi inapaswa kupata ushindi kwenye mchezo wake wa mwisho wa kundi D dhidi ya US Gendarmerie ili afikishe alama 10 na aungane na mshindi kati ya RS Berkane na ASEC mimosas Aprili 1,2022.

Simba SC ikitokea imepata sare na RS Berkane akafungwa na ASEC Mimosas basi Simba SC itakuwa na alama 8 na Berkane kubakia na alama 7 hivyo Wekundu wa msimbazi watauzu. Ikitokea Simba akatoa sare na Berkane akashinda, hawatofuzu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live