Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wamuwahi mtani kwa Mkapa

Simba Zanzibar  Sehemu ya wachezaji wa Simba SC

Sun, 23 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Simba kimewawahi wenyeji wao Yanga kutua uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam tayari kwa mchezo wa ligi kuu mzunguko wa kwanza.

Kikosi hicho kimefika saa 9:17 alasiri huku nahodha msaidizi wa timu hiyo, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ akiwaongoza wachezaji wenzake kwa kuanza kushuka.

Kikosi hicho kiliingia na kupokelewa na makomandoo wa Simba ambao waliwatawanya mashabiki waliokuwa eneo hilo ili kulipisha gari ya timu hiyo iliyokuwa imebeba wachezaji.

Mastaa wa Simba na benchi la ufundi walitumia dakika tatu tu kushuka kwenye gari hiyo na kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo tayari kwaajili ya kujiandaa na mchezo.

Phiri, Mayele watajwa kwa Mkapa

Mahabiki wa Yanga na Simba wamekuwa na matumaini makubwa ya timu zao kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa leo huku nyota wao Moses Phiri na Fiston Mayele wakionekana kuteka hisia zao kwa wingi.

Baadhi ya mashabiki wa Simba wamekuwa wakimtaja mchezaji wao, Moses Phiri kama ndiye atakayewapatia ushindi muhimu leo kutokana na kiwango bora ambacho amekuwa nacho.

Kwa upande wa Yanga nao hali ni hiyo hiyo kwa Fiston Mayele ambaye tangu amejiunga na Mabingwa hao watetezi amekuwa na mchango mkubwa kwenye kuzifumania nyavu.

Phiri ambaye alikosa Dabi iliyopita kwenye Ngao ya Jamii Agosti 13, mwaka huu waliyofungwa 2-1 amekuwa kwenye kiwango kizuri chini ya Kocha, Juma Mgunda huku akifunga mabao manne ya Ligi Kuu Bara hadi sasa.

Wakati mashabiki hao wakipewa motisha na Phiri, Mayele ndiye anayeonekana tishio zaidi kwa Simba kwani anakumbukwa kwa kuwafunga mabao yote mawili kwenye ushindi wa 2-1 katika Ngao ya Jamii mara ya mwisho walipokutana.

Mbali na Mayele kukumbukwa kwa hayo ila pia msimu huu tayari ameweka kambani mabao matatu kwenye Ligi Kuu Bara akiifukuzia rekodi yake ya msimu uliopita alipofunga mabao 16, nyuma ya kinara, George Mpole wa Geita Gold aliyemaliza na 17.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live