Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wamtaka Mouhsine Bodda

Mouhsine Bodda Mouhsine Bodda

Thu, 30 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taarifa za ndani kabisa zinaeleza kuwa Simba SC ipo tayari kumpa Mohsen Bodda mshahara wa USD 8,000 ambazo ni sawa na zaidi ya Tsh Million 20 kwa mwezi.

Nyota huyo anataka kuondoka FC Nouadhibou ya nyumbani kwao Mauritania baada ya msimu huu kumalizika na hilo lilithibitishwa na Kocha wa timu hiyo Artiz Lopez Garai wiki kadhaa zilizopita.

Mbali na Simba SC pia Al Hilal, Al Merreikh zote za nchini Sudan pamoja na baadhi ya klabu kubwa nchini Morocco zimekuwa zikihusishwa na Bodda aliyeisaidia FC Nouadhibou kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu huu 2023/24.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live