Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wamtaka Lameck Lawi arudishe pesa zao

Lameck Lawi Simba Coastal Simba wamtaka Lameck Lawi arudishe pesa zao

Wed, 4 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba SC wameweka wazi hawamuhitaji tena Lameck Lawi ambaye amerejea nchini baada ya kufeli majaribio yake Ulaya

Simba wamebariki mchezaji kusalia Coastal Union kikubwa arudishe Pesa zote alizoingiziwa kama Signing fees.

Simba wamekubali kutumia busara kama ambavyo kamati ilitaka suala limalizwe kwa busara, Wameachana na mchezaji ambae alikua wao kihalali kimkataba.

Baada ya Israel Patrick sasa ni Lameck lawi, Kikubwa mzigo urudi kila mtu aendelee na maisha yake.

Baada ya kurejea nchini, beki Lameck Lawi amesema hatma ya yeye kuitumikia Coastal Union ipo chini ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya Simba kuendelea kukomaa.

Lawi ambaye alisaini mkataba ndani ya Simba, ameshindwa kuitumikia timu hiyo na badala yake alitimkia Ubelgiji kwa ajili ya kujaribu kwenye klabu ya K.A.A Gent lakini mambo yameenda tofauti, hivyo amerudi Tanzania

Lawi akizungumzia namna mchakato wake wa usajili ulivyoenda amesema anapitia wakati mgumu sasa kutokana na kukosa nafasi ya kucheza kuendeleza alipoishia msimu uliopita na hatimaye kufikia malengo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live