Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wamkana Muharami sakata la Madawa

Simbaaaa Madawa Taarifa ya Simba SC

Tue, 15 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Klabu ya Simba unaujulisha umma kuwa aliyekua Kocha wa magoli kipa Muharami Said Mohammed maarufu Shilton hakua muajiriwa wa klabu hiyo na wala hakua na mkataba na Simba.

Simba ilimuomba Muharami kuwanoa makipa wake kwa muda kwa mwezi mmoja, wakati huo klabu ikiendelea kutafuta Kocha wa kudumu.

Kwa mantiki hiyo klabu haihusiki na tuhuma zinazomkabili Kocha huyo na klabu iko tayari kutoa ushirikiano kwa mamlaka husika pindi itakapohitajika kwa maslahi ya Taifa.

Uongozi wa Simba unawaomba mashabiki wa klabu hiyo kuwa watulivu kwani hakuna athari yeyote kwa klabu kutokana na kadhia iliyomkumba Kocha huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live