Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wamesajili vizuri lakini kwa Yanga hii nalala fofofo - Eng. Hersi

Hersi X Gamondi  Simba wamesajili vizuri lakini kwa Yanga hii nalala fofofo - Eng. Hersi

Thu, 22 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi amepongeza usajili ambao watani zao Simba SC wameufanya kwenye msimu huu lakini akasema kwa kikosi alichonacho yeye wala hawezi kukosa usingizi sababu ya Simba.

Hersi amesema hayo wakati akizungumza na Wasafi Media kuhusu masuala mbalimbali ya klabu hiyo.

“Simba wana timu nzuri, maboresho yamefanyika na jitihada kubwa zimefanyika kusajili wachezaji wapya, viongozi wanapaswa kupongezwa kwa hilo. Kuna uwekezaji mkubwa umekwenda pale, tumeambiwa wametumia zaidi ya Tsh bilioni 7, na kuna maingizo mengine mapya ambayo yameongeza thamani ya Tsh bilioni 7, wanapaswa kupongezwa.

“Kwenye matokeo watakayoyapata Simba uwanjani inatokana na mambo mengi, mwalimu, wachezaji kuungana, kupambania timu, kuhamasika ili kuleta matokeo hayo yote yanaweza kuleta matokeo ya mwisho. Ninawapongeza kwa usajili waliofanya, kikubwa ni kuendelea kuijenga timu yao ili iweze kuleta matokeo wanayoyatamani.

“Simba wana wachezaji wengi wazuri, lakini nimemuona Edwin Balua, ameonesha kitu kizuri, ni Mtanzania mwenzetu na ninaendelea kumtia moyo aongeze bidii ilikusogeza mbele kipaji chake.

“Simba haiwezi kuninyima usingizi hata siku moja. Yani Yanga hii na Simba hii nisipate usingizi? Yanga hii ya Gamondi, Diarra, Yao, Boka, Job, Bacca, Mwamnyeto, Aucho, Maxi, Pacome, chagua wewe aanze Chama au Aziz KI,” amesema Hersi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: