Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wamempa Kibu thamani kubwa kuliko uwezo wake - Geoff Lea

Kibu Denis Prosper Simba wamempa Kibu thamani kubwa kuliko uwezo wake - Geoff Lea

Thu, 2 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitia EFM, Kamanda Geoff Lea anasema kiwango cha Kibu Dennis kimeshuka tangu ajiunge na Simba SC akitokea Mbeya City.

Geoff anaamini kwamba ni tatizo kwa ukubwa wa Simba SC kutegemea mchezaji kama Kibu peke yake na ndilo eneo ambalo Yanga Sc wanawazidi Simba kwenye kufanya maamuzi magumu dhidi ya wachezaji ndiyo maana mchezaji huyo amewavimbia mabosi wa Msimbazi kusaini kandarasi mpya.

“Kama tukiwa wakweli, Kibu hajawa na best performance kama aliyokuwa nayo kabla ya kwenda Simba ambayo iliwashawishi Simba kumleta ndani ya klabu yao. Fact ni kwamba uwezo wa Kibu umekuwa ukishuka tangu aje Simba.

“Kibu akiwa Mbeya City alifunga mabao 8, alihusika kwenye mabao kama 15 hivi, alipotua Simba msimu wa kwanza bao 7, kiwango cha kawaida, msimu huu ana bao moja pekee. Uwezo wake umeshuka sana anatakiwa aambiwe ongeza bidi. Uwezo wake haujafika kule ambako Simba walidhani angeweza kufika. Unaweza kuihusisha hiyo na matatizo yalipo Simba ndiyo maana wapo tayari kuendelea naye.

“Kama timu kubwa kama Simba inapofikia wakati wanamtegemea mchezaji kama Kibu basi kuna shida. Eneo ambalo Yanga wanaizidi Simba ni kufanya maamuzi magumu. Walimtoa Yanick Bangala akitoka kuwa MVP, Djuma Shabani, Saido Ntibazonkiza wakiwa na kiwango bora na sasa wanamuacha Joyce Lomalisa, wote hawa wameachwa kwa sababu ya mambo kama haya.

“Simba wamempa Kibu Denis thamani ambayo yeye ameonesha labda anastahili thamani kama ile, na ameonesha ishara kuwa anataka kuondoka. Kwenye makubaliano ya mkataba ametaka mwanasheria wake awepo akaletwa, meneja wake akaletwa, akataka kaka yake yupo Kigoma, tafsiri ni kwamba huyu mtu hataki kuwepo kwenye klabu,” amesema Jeof.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: