Mchezaji wa zamani wa Taifa Stars na vilabu vya Yanga na Simba, Bakari Malima 'Jembe Ulaya' amesema kuwa, iwapo klabu ya Simba inataka kufanya vizuri kimataifa, wanapaswa waachane na baadhi ya wachezaji kwani wanaonekana hawana kipya cha kuisaidia timu yao.
Jembe Ulaya amesema kuwa, Simba wamebweteka na mafanikio ya kufika hatua ya makundi kwenye michauno ya kimataifa kila mwaka, hivyo wameshindwa kuboresha kikosi chao ili wafanya vizuri na badala yake wameridhika na mafanikio hayo madogo wanayoyapa.
"Simba kwa miaka mine mitano wamesha-prove kwamba suala la group stage kwao ni kawaida, lakini wamebweteka na group stage hawajataka kubadilika kuleta wachezaji bora zaidi. Wameleta kocha bora Benchikha mwenye wasifu mkubwa.
"Sasa hivi wasiwe na uharaka sana wa kulazimisha Benchikha aipeleke timu kwenye robo fainali na nusu fainali kwa kikosi alicho nacho. Ni muda muafaka wa kumwachia Benchikha timu aitengeneze kwa ajili ya kwenda robo fainali na nusu fainali.
"Simba wasiende na historia ya wacheaji kwamba alikuwa hivi akija hapa atatusaidia, wanatakiwa wafungue pochi waende kwa wachezaji ghari wenye ubora, naamini watafanya vizuri sana kwa sababu tayari wameshaonyesha kwa kiasi flani ufalme kwenye soka la Afrika," amesema Jembe Ulaya.