Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba walivyoibeba Namungo

Simba+pic Simba walivyoibeba Namungo

Wed, 30 Sep 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By THOBIAS SEBASTIAN NA OLIPA ASSA PAMOJA na Kocha wa Namungo, Hitimana Thierry kukaririwa akisema asilimia kubwa ya usajili uliofanywa msimu huu hayakuwa matakwa yake, wapo wachezaji ambao kwa uzoefu wao wanaweza wakasaidia timu hiyo kwenye, Kombe la Shirikisho Afrika.

Msimu uliopita Thierry alikuwa na kikosi kizuri kilichoisaidia timu hiyo, kumaliza nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, akiwemo Reliants Lusajo aliyemaliza na mabao 13 na sasa kahamia (KMC), LucaS Kikoti na Bigirimana Blaise hao bado wapo.

Katika usajili wa msimu huu kuna mastaa wapya ambao wamekwenda kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho na wana uzoefu wa kucheza michuano ya kimataifa na ligi ya ndani, hivyo uwepo wao utaibeba timu hiyo.

HARUNA SHAMTE

Alitamba akiwa na Simba kwa misimu mitatu mwaka 2011 mpaka 2014, kabla ya kwenda JKT Ruvu, kisha Mbeya City na Lipuli.

Simba ilimsajili tena msimu uliopita kwa mwaka mmoja kabla ya kuvunja mkataba wake kutokana na kukosa nafasi mbele ya Shomary Kapombe na sasa amejiunga na Namungo kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz