Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba walikosea kumleta Robertinho - Mchambuzi

Robertinho Yangaaaa Simba walikosea kumleta Robertinho - Mchambuzi

Wed, 8 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa soka kutoka EA Radio, Abissay Stephen amesema kuwa Klabu ya Soka ya Simba ilifanya makosa makubwa kumsajili Robertinho kama kocha wao mkuu kwani walisaliti falsafa ya soka lao la kupiga pasi.

Robertinho amefurushwa ndani ya Simba Sc baada ya kufungwa bao 5-1 na wapinzani wao, Yanga katika mchezo wa juzi Novemba 5, 2023 katika Dimba la Mkapa.

"Simba kumchukua Robertinho walisaliti philosophy yao ya Lunyasi, kwa sababu Robertinho sio muumini wa hivyo, wao ndio walikosea kumleta Robertinho.

"Robertinho yeye yupo sahihi kwenye mbinu zake kwa sababu hizo ndizo zilimpa mafanikio yeye hadi Simba kumtaka, sasa leo huzitaki mbichi hizi yaani its very funny unajitekenya halafu unacheka mwenyewe.

"Mfano kocha wa Yanga Miguel Gamondi, Yanga wali-Scout kweli, kuna mpira Nabi aliuacha wa Possession, Yanga walitaka ku-maintain aina hiyo ya mpira.

"Wamekutana na Gamondi wamemchunguza walivyoona wakasema basi wewe tukuchukue utaweza, Gamondi si ndiyo huyu sasa, sasa hivi yeye kaongeza ile attacking flow yao imekuwa ya speed kiasi, hebu ona Yanga wanavyomwaga, sasa kwa Simba yule aliyesema Robertinho njoo Simba wakamuhoji huyo huyo," amesema Abissay Stephen.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live