Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba walifeli hapa kwa Mashujaa

Simba Mashujaa Msis Simba walifeli hapa kwa Mashujaa

Wed, 10 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nafikiri hii ndio mechi ambayo Simba alicheza kwa intensity ya hali ya chini zaidi, pressing ilikuwa dhaifu sana, kushinda mipambano yao ilitegemea na mistakes za Mashujaa kukosea kupiga pass au kuclear mpira.

Kuna wakati walikuwa wamesinzia Mashujaa ni basi tu hawakuwa wakatili golini , hawakutoa adhabu stahiki.

Mashujaa kwa kushinda kutoa adhabu stahiki kwa Simba kusinzia sana hasa kipindi cha kwanza, naona Simba walishukuru hilo.

Mashujaa hawakufanya high pressing bali waliwasubiri Simba kuja kwenye zone yao ambapo Zuber Dabi, Omary Omary na Balama Mapinduzi waliwin balls kwa kiwango kikubwa na kushinda mipambano ya utatu wa Sarr, Ngoma na Chama.

Well Mashujaa walikuwa watulivu sana, waligundua huwezi kupishana na Simba inakupasa uweze kucheza chini na kuanza build up ya haraka sana kwasababu Simba walikuwa wanaacha distance na space kubwa sana kwenye mistari yote mitatu (Ushambuliaji, Viungo, Ulinzi) energy yao ilikuwa nzuri muda wote licha ya kuwa kupungukiwa mchezo mmoja kwa dakika kadhaa. Upigaji mzuri wa penati umewapa ufunguo wa matokeo!

Dondoo

1: Balama ni bonge la kiungo, ndio alikuwa anaipa control nzuri sana Mashujaa

2: Mo Hussein ni bora sana , always available mchezoni

3: Johora alikuwa mtulivu, alifanya save nyingi kwa uzuri ambazo unaweza kuziona rahisi

4: Jobe mh anakupa mechi nzuri halafu mechi nyingi anakuweka kabatini

5: Adam Adam ni mshambuliaji hatari sana, combination play yake na Dabi ni nzuri.

6: Mashujaa wale Robo fainali

FT: Mashujaa 1-1 Simba PEN (6-5)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live