Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wakitaka mafanikio wawatimu Chama, Saido, Ngoma

MO NA CHAMA Simba wakitaka mafanikio wawatimu Chama, Saido, Ngoma

Fri, 17 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Inaelezwa kuwa, Simba SC ili iweze kufanikiwa na kurudi kwenye hali bora ni lazima iachane na wachezaji ambao umri umeenda (veterans) akiwemo Chama, Saido na Ngoma.

Akizungumza kwenye Sport Arena ya Wasafi, mchambuzi Nasri Khalfan, amesema kiwango kinaoochenywa na wachezaji hao kwa sasa haitakiwi kuwalaumu kwasababu ni hali halisi kutokana na umri kuwatupa mkono.

"Hivi sasa Simba wapo kwenye nyakati za kumruhusu kila mchezaji ambae hataki kubaki kwenye ile Klabu aende.

"Hawa wachezaji wanaoisumbua Simba ama wanahisi wapo sehemu ya kisumbua Simba ili wabaki kwenye hiyo Klabu ndio hawa hawa ambao wapo kwenye hiyo Klabu takribani misimu mitatu na Simba haijatwaa taji lolote la maana.

"Kwa hiyo hai guarantee chochote kwamba, Chama sijui Inonga, Kibu Denis, kama wakibaki Simba ndio itarejesha utawala wao, hai-guarantee hicho kitu.

"Chama alishafanya kazi kubwa miaka iliyopita na alishaifanya Simba kutawala huu mpira kwa hiyo lazima viongozi wa Simba wakubali kwamba,kuna wachezaji nyakati zao zimeshapita.

"Hivi sasa Chama yupo sehemu ambayo haonekani kama anaweza kuipambania Klabu kwa misimu mitatu, ameshaanza ku drop sasa mpigie misimu mitatu.

"Simba waingize vijana wengine wapya ambao wataibeba project kwa misimu mitatu mbele lakini wakisema wawang'ang'anie hawa hawa ma veteran ambao wameshaikwaamisha Simba Kwa misimu mitatu watakuwa wanajirudisha nyuma.

"Saidoo ni veteran,katika kipindi cha miezi amabacho walimchukua kutokea Geita, walitakiwa wamtumie Saido pale tu labda na msimu ule wa nyuma lakini wao wakafanya ni usajili wa muda mrefu.

"Wameenda kumchukua Ngoma, yule ni veteran ameshakuwa kwenye peak yake toka yupo Morocco, Sudan huko, hapa amekuja kumalizia na hata ukimuangalia jinsii anavyocheza, angalia Simba ikipoteza mpira hata energy ya ku recover hana yupo zake jogging na utamlaumu nini kwa mchezaji ambae ameshakuwa kwenye peak yake na sasa ana drop hana tena deni kwenye career yake.

"Chama pia anaonekana anaelekea huko alishakuwaga kwenye peak yake kwa hiyo hawezi tena kuwa Chama yule wa misimu mitatu iliyopita, alishaendaga hadi Morocco amerudi na sasa anaonekana ana decline, Simba wasing'ang'anie," amesema Nsir.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live