Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wakiri kuomba kucheza na Coastal wiki hii

Kama Hujanunua Tiketi Usiende Uwanjani   Ahmed Ally Simba wakiri kuomba kucheza na Coastal wiki hii

Wed, 23 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wekundu wa Msimbazi Simba SC, wamekiri kuwaandikia bodi ya Ligi barua ya kuomba wacheze raundi ya tatu mechi dhidi ya Coastal Union.

Akizungumzia suala hilo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema Bodi ya Ligi waliuweka 'pending' mchezo huo wakidhani Simba wataanzia hatua ya awali katika michezo ya Kimataifa lakini bahati nzuri hawakuanzia.

"Ilikuwa tusicheza raundi ya tatu kutokana na kudhani tutaanzia hatua ya awali Klabu Bingwa lakini bahati nzuri hatukuanzia hatua hiyo.

"Ukiangalia ratiba tuna mchezo mwingine tarehe tatu mwezi wa kumi. Tumeomba watupe mechi na Coastal Union ili kuepuka viporo huko baadaye. Bodi nadhani wataangalia na wenzetu nafasi yao ili kama wana nafasi nzuri basi tutacheza watakapoturuhusu, sisi tupo tayari na ndio maana tukaomba tupangiwe wiki hii," alisema Ahmed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live