Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba waja na 'vita ya kisasi' dhidi ya Jwaneng Galaxy

Ahmed Ally: Twendeni Uwanjani Hata Kama Tuna Hasira.jpeg Simba waja na 'vita ya kisasi' dhidi ya Jwaneng Galaxy

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema mashabiki wa klabu hiyo wanapaswa kuwa sehemu ya kufuzu hatua ya robo fainali Machi 02, 2024 dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana kwa kufika kwa wingi uwanjani.

Katika mchezo huo wa hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL), mnyama anahitaji ushindi ili kutinga hatua ya robo fainali kwa mara ya nne katika historia.

"Tumezoea kwenda robo fainali, kwahiyo ni lazima tutinge robo fainali. Na hili inapaswa kufanyika kwa pamoja." Amesema Ahmed.

Simba wana kumbukumbu mbaya ya Oktoba 24, 2021 ambapo waliingia Uwanja wa Benjamin Mkapa ikiwa na kumbukumbu ya ushinda ugenini Botswana kwa mabao 2-0 lakini Watswana hao wakapeleka kilio Msimbazi kwa kumchabanga mnyama 3-1 hivyo kuhitimisha safari ya mnyama.

Simba wapo kundi A la CAFCL, wakiwa nafasi ya pili kwa alama 6 wakifungana na Wydad AC walio nafasi ya tatu. Galaxy wanaburuza mkia wakiwa na alama 4 huku Asec Mimosa vinara wa kundi wakiwa na alama 11 huku wakiwa tayari wameshafuzu hatua ya robo fainali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live