Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba waja na Mkakati tatizo la kutofunga magoli, Pablo anyoosha maelezo

Magoli Simba (600 X 400) Simba waja na Mkakati tatizo la kutofunga magoli

Fri, 11 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya kwamba mastraika wa Simba wameendelea kulaumiwa kwa kuinyima ushindi timu hiyo katika mechi mfululizo walizocheza, kocha wa kikosi hicho, Pablo Franco ameshtukia jambo na kulifanya kazi haraka kabla ya kukutana na Asec Mimosas.

Mashabiki wa Simba na wadau wa soka wamepatwa na wasiwasi na safu ya ushambuliaji ya Simba inayoelekea kuikabili miamba hiyo ya Ivory Coast kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaofanyika Jumapili kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, kocha Pablo anajua majanga ya safu yake ya ushambuliaji na sasa ameamua kuja na mbinu mbadala ya kuwataka wachezaji wote wa kikosi hicho wakiwemo mabeki kufunga mabao huku akisema soka la sasa limebadilika.

Pablo alisema ni mbaya kwa timu kutegemea mtu mmoja au wawili wawafungie mabao kwani madhara yake ni makubwa kwa sababu wakidhibitiwa inaweza kuwapa wakati mgumu, “Tunapaswa kuwa timu ambayo haitabiriki.

“Kitu muhimu ni kuendelea kutengeneza nafasi na kujitahidi kuzitumia, kila mchezaji ana wajibu wa kutufungia bao, mpira siku hizi umebadilika wapo mabeki wenye idadi kubwa ya mabao,

“Najua hali ilivyo lakini hicho sio kisingizio kwetu tunapaswa kuimarika katika utumiaji wa nafasi si kwa washambuliaji pekee bali kwa mtu yeyote atakayepata nafasi,” alisema Pablo

Katika mazoezi yaliyofanyika juzi jioni kwenye Uwanja wa Mo Simba Arena uliopo Bunju, Pablo aliwaongoza wachezaji wachache kufanya mazoezi, wale ambao hawakucheza kabisa mechi iliyopita ya ligi dhidi ya Mbeya Kwanza na walioingia kutokea benchi wakati wale waliocheza dakika zote 90 walipewa program maalum ya Gym.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live