Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba waivimbia TFF, yaandika barua kutaka ufafanuzi wa Mkataba wa GSM

Simba Yavimba CEO wa Simba ,Babra Gonzalez akiwa na Magori

Tue, 7 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ligi Kuu Tanzania Bara 2021/2022 ina wadhamini wawili, Benki ya NBC ambae ndie mdhamini mkuu, lakini GSM ni mdhamini mwenza.

Kanuni za Shirikisho la Mpira zinahitaji kila timu kuvaa nembo ya mdhamini katika jezi zake inaposhiriki michezo ya Ligi.

GSM pia ndio mdhamini wa Yanga, na anafanya kazi kwa karibu na Yanga bila kuvisahau vilabu vya Namungo na Coastal Union.

Sasa Disemba 11 miamba hii itakutana katika mchezo wa Ligi Kuu, na kama kanuni zinavyohitaji Simba itawalazimu kuvaa jezi zenye nembo ya GSM.

Sasa katika suala hilo ndipo ambapo Simba imeiandikia barua TFF na Bodi ya Ligi kutaka ufafanuzi wa Mkataba huo baina ya TFF na GSM.

miongoni mwa yale wanayoyataka kujua Simba na kwa ufupi kutoka katika barua hiyo wanasema

"Sisi kama Simba tunapenda kupewa ufafanuzi juu ya Mkataba wa Udhamini wa Ligi kuu ambao Bodi ya Ligi imeuingia na Kampuni ya GSM,huku matakwa makuu yakiwa nikuweka chapa za GSM katika jezi za vilabu..

Pia Simba inaona kama kama kuna mgongano wa kimaslahi Kwa sababu GSM amemdhamini Yanga ambaye Kimsingi kakosa Ubingwa miaka minne iliyopita Huku Simba akichukua.

Simba tunataka ufafanuzi juu ya kwanini viongozi wa klabu ya Yanga walikuwa katika utiwaji Saini wa Mkataba baina ya TFF/TPLB na Kampuni ya GSM.

Akizungumza MweNyekiti wa Simba Murtaza Mangungu kutilia mkazo sakata hilo amesema;

"Hilo suala la huo Mkataba TFF walishatoa taarifa kuwa ni suala lao, lakini sisi tumeandika barua kutaka maelezo ambayo ni haki yetu"

"Tuna hoja nyingi ambazo nikianza kuzielezea tunaweza tukaingia kwenye mlango mwingine ambao sitapenda kuufikia, ila sisi tumetoa maelezo yetu na tumeshayawasilisha kwao tukitaka maelezo baina ya TFF na huyo mdhamini juu ya huo mkataba.

"Sisi kama wadau ni haki yetu kuhoji, kuuliza na kutaka ufafanuzi pale unapoona unapaswa" amesema Mangungu

Novemba mwaka huu TFF, iliingia Mkataba wa udhamini mwenza wa Ligi Kuu na GSM, Mkataba wenye thamani ya Bilioni 2.1 kwa muda wa miaka miwili.

Kwa mujibu wa kanuni timu itakayogomea kuvaa nembo ya mdhamini watapigwa adhabu za aina tofauti tofauti ikiwemo faini ama kushushwa daraja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live