Baada ya kumalizika kwa msimu wa 22/23 wa mashindano ya CAF ngazi ya Klabu, Shirikisho la soka Afrika limeweka hadharani Viwango vya Klabu zilizofanya vizuri katika michuano yake kwa miaka mitano iliyopita huku Simba SC ya Tanzania ikifanikiwa kushika nafasi ya 9.
1. Al Ahly — 83 points 2. Wydad — 74 points 3. ES Tunis — 56 points 4. Sundowns — 51 points 5. Raja CA — 51 points 6. Zamalek — 39 points 7. RS Berkane — 37 points 8. CR Belouizdad — 36 points 9. Simba — 35 points 10. Pyramids — 35 points
Ikumbukwe Simba SC imecheza robo fainali 3 za Klabu bingwa na moja ya Kombe la Shirikisho na hicho ndicho kigezo kilichowapa nafasi ya kuorodheswa ndani ya Klabu bora kwa miaka mitano.
USMA imefanikiwa kutwaa Ubingwa wa Shirikisho lakini haipo hata kumi bora, lakini Simba hata nusu fainali hawajafika wapo kumi bora, maana yake ili utajwe hapo lazima uwe na kiwango bora chenye muendelezo katika michuano hii.