Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba waingia kambini fasta kuwawinda Al Ahly

Simba Waingia Kambini Fasta Kuwawinda Al Ahly Simba waingia kambini fasta kuwawinda Al Ahly

Mon, 18 Mar 2024 Chanzo: Mwananchi

Baada ya mapumziko ya siku mbili, Simba inarejea kambini leo Jumatatu lakini tayari imeanza kupiga hesabu mbili muhimu kabla ya kuikaribisha Al Ahly ya Misri kwenye mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, itakayopigwa Machi 29 mwaka huu, Uwanja wa Benjamin Mkapa, kuanzia saa 3:00 usiku.

Simba na Yanga zimefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali kwenye michuano hiyo mikubwa zaidi kwa upande wa klabu Afrika.

Hesabu ya kwanza kwa Simba ni kuweka kambi fupi Unguja, Zanzibar kabla ya kuwakabili Al Ahly. Hii imekuja baada ya kocha mkuu wa timu hiyo, Abdelhak Benchikha kuwaambia viongozi wa timu hiyo anataka kikosi chake kiwe pamoja na kukaa kwa utulivu zaidi.

Kiongozi mmoja wa Simba ameliambia Mwananchi, jambo hilo litafikiwa muafaka leo jioni baada ya kikao cha viongozi na benchi la ufundi. Jambo la pili ambalo Simba inapigia hesabu ni namna ya kuwapata kwa wakati wachezaji wake walioitwa kwenye timu za taifa.

Mastaa Aishi Manula, Kibu Denis, Keneddy Juma na Mohamed Hussein 'Tshabalala' wameitwa Taifa Stars huku Mzambia Clatous Chama akiitwa Chipolopolo na Saidi Ntibanzokiza akiitwa kwenye kikosi cha Burundi.

Chanzo: Mwananchi