Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba waichimba mkwara Kaizer Chiefs

D64803ee3d6d1d2bb1ac77cabec4cd02.jpeg Simba waichimba mkwara Kaizer Chiefs

Thu, 13 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KIUNGO mshambuliaji wa timu ya Simba, Clatous Chama amesema kuwa malengo yao msimu huu ni kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hivyo Kaizer Chiefs wasitarajie mteremko katika mchezo wa kwanza wa robo fainali.

Simba wanatarajia kushuka Jumamosi wanatarajia kushuka kwenye Uwanja wa FNB Afrika Kusini kuwakabili wabishi Kaizer Chiefs, ambao wametinga hatua ya robo fainali wakitokea Kundi C.

Akizungumza jana na gazeti hili, Chama alisema kuwa licha ya kuwa mchezo huo unatarajiwa kuwa na upinzani wa hali ya juu kwa timu zote mbili, ambazo zina malengo kutinga hatua inayofuata ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hivyo hawatakubali kupoteza mchezo huo licha ya kuwa ugenini.

“Tumekuja Afrika Kusini kutafuta matokeo ili kujiweka katika nafasi nzuri tutakaporudi nyumbani katika mchezo wa marudiano ambao ndio utatoa hatima ya nani aende nusu fainali.

“Haikuwa jambo rahisi kumaliza nafasi ya kwanza mbele ya bingwa mtetezi, ambaye ni kinara katika orodha ya timu bora Afrika, tumekuja huku kupambana kila mchezaji kiu yake ni kuona tunacheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika,” alisema Chama.

Chama alisema kuwa ubora wa kikosi chao unatokana na malengo waliyojiwekea na umoja uliopo, ambacho kimekuwa na muendelezo mzuri wa matokeo kuanzia katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na Kombe la Shirikisho la Azam.

Naye Meneja wa kikosi cha Simba, Patrick Rweyemamu alisema kuwa wanaendelea vizuri na mazoezi, lakini mlinzi wao Paschal Wawa na kocha wa viungo Adel Zrane, wamekwama nchini Kenya kutokana na matatizo katika pasipoti zao, hivyo hawajaungana timu.

Chanzo: www.habarileo.co.tz