Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wahamishia nguvu Kombe la Shirikisho la Azam

Kikosi Simba SC 1140x640 Simba wahamishia nguvu Kombe la Shirikisho la Azam

Mon, 27 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mara baada ya kurejea nchini wakitokea nchini Uganda, Wekundu wa Msimbazi Simba SC, akili yao wameielekeza kwenye Kombe la Shirikisho la Azam ambapo wanatarajia kushuka Uwanjani Machi 2, 2023.

Simba wanatarajia kupepetana na African Sports kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam baada ya kutoka Uganda walikoibuka na ushindi wa goli 1-0.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Simba SC, wachezaji walipewa mapumziko ya siku moja (Februari 26) na leo (Februari 27) wanarejea mazoezini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo wa Htaua ya 16 Bora.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live