Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wafunguka sababu Miquissone kukosa mchezo wa Power Dyamos

Jose Luis Miquissone Dau Simba wafunguka sababu Miquissone kukosa mchezo wa Power Dyamos

Wed, 4 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba SC wameeleza sababu ya Luis Miquissone kuukosa mchezo wa pili wa Klabu Bingwa dhidi Power Dynamos uliochezwa Jumapili iliyopita katika Uwanja wa Azam Complex-Chamazi jijini Dar.

Akizungumza na Wasafi FM, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally alisema, Miquissone alipata shida kidogo kwenye mguu ambapo daktari alishauri apumzike ili kumlinda asiweze kuumia zaidi.

"Alipata shida kidogo kwenye mguu, daktari akashauri apumzike ili asije kupata maumivu zaidi lakini kwa sasa yupo fiti na atakuwa sehemu ya kikosi kilichoenda Mbeya kuwakabili Tanzania Prisons," alisema Ahmed.

Mchezo huo Simba walifanikiwa kushinda na kufuzu hatua ya Makundi baada ya kutoka sare ya 1-1 na kupata faida ya goli ala ugenini. Wakiwa ugenini Zambia, Simba walitoka sare ya 2-2.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live