Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wafunguka madai ya Phiri kuondoka Simba

Simba Wafunguka Madai Ya Phiri Kuondoka Simba Simba wafunguka madai ya Phiri kuondoka Simba

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba SC wamezungumzia madai ya straika wao Mosses Phiri kuwa ataondoka kwenye dirisha dogo la usajili.

Akizungumzia mchezo wa dabi ya Jumapili hii, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema Phiri bado yupo sana Msimbazi.

"Tetesi za Moses Phiri kuondoka kwenda Yanga SC au timu nyingine niwambie tu wataendelea kumtamani kama wanavyotamani wachezaji wengine. Moses ataondoka Simba siku tukiamua kuachana nae na siku hiyo siioni, hawatampata General hata siku moja."

"Kwanza Moses Phiri anaondokaje Simba. Simba ni sehemu ya wachezaji kutimiza malengo yao, wachezaji wetu ni matajiri, wanaishi maisha ya kifalme."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live