Wed, 22 Feb 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Kufuatia uvumi uliosambaa mitandaoni kuwa Kocha wa Simba SC, Roberto Oliviera 'Robertinho' kuwa amesitishiwa mkataba, uongozi wa Wekundu hao wa Msimbazi wameibuka na kukanusha.
Simba wamekanusha suala hilo kupitia ukurasa wao wa Instagram, ambapo wameandika hivi:
"Taarifa zinazosambaa mitandaoni kuhusu mkataba wa Kocha Robertinho sio SAHIHI. Anaendelea na majukumu yake ya kuandaa kikosi kuelekea mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika."
Simba wanajiandaa kucheza mchezo wao wa tatu wa hatua ya Makundi ya Klabu Bingwa dhidi ya Vipers ya Uganda, Jumamosi Februari 25, 2023.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live