Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wafunga mwaka kibabe, Bocco, Saido waiteka shoo kwa Mkapa

Bocco X Saido Taifa Bocco, Saido waiteka shoo kwa Mkapa

Fri, 30 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wekundu wa Msimbazi Timu ya Simba wameshusha mvua ya magoli kwa maafande wa jeshi la magereza Timu ya Tanzania Prisons.

Mchezo huo wa raundi ya 19, uliopigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam uliwashuhudia Simba wakiibuka na ushindi wa mabao 7-1 mbele ya maafande wa Prisons.

Magoli ya Simba katika mchezo wa leo yamefungwa na John Bocco aliefunga mabao matatu (Hat-Trick), Said Ntibazonkiza aliefunga mabao matatu (Hat-Trick) na beki Shomari Kapombe.

Goli pekee la Prisons limefungwa na Jeremiah Juma dakika ya 29, huku Prison wakimaliza mchezo huo wakiwa pungufu baada ya Samson Mbangula kuoneshwa kadi nyekundu kipindi cha kwanza.

Mbali na ushindi huo, habari kubwa ni Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Saidi Ntibazonkiza aliyesajiliwa katika dirisha dogo la usajili na kuanza mchezo wa leo ni kupachika mabao matatu na kutoa pasi moja iliyozaa goli.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live