Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wachukua alama tatu mbele ya Vipers kwa Mkapa

Chama Vs Vipers Clatous Chama akimiliki mpira mbele ya wachezaji wa Vipers

Tue, 7 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wawakilishi wa Tanzania katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, Timu ya Simba SC imefanikiwa kuondoka na alama tatu muhimu dhidi ya Vipers ya Uganda.

Mchezo huo wa Hatua ya Makundi umepigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Bao pekee la ushindi katika mchezo huo limefungwa na kiungo Clatous Chotta Chama dakika ya 45+1.

Kwa ushindi huo Simba wanakwea mpaka nafasi ya pili katika msimamo wa kundi C, hivi sasa wakiwa na alama 6 nyuma ya Raja Casablanca.

Mpaka sasa msimamo upo hivi;

KUNDI C

1. Raja Casablanca — 12pts

2. Simba SC — 6pts

3. Horoya AC — 4pts

4. Vipers SC — 1pts

Chanzo: www.tanzaniaweb.live