Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wachukua alama 3 muhimu mbele ya Vipers Uganda

Kanoute Vs Vipers Simba imeibuka na ushindi wa bao 1-0

Sat, 25 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dakika 90 zinakamilika katika Uwanja wa St Marys Uganda, mchezo wa hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, Kundi C.

Simba wanafaikiwa kuondoka na alama tatu na kufufua matumaini ya kutinga hatua ya Robo Fainali ya michuano hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 ugenini.

Bao la Simba katika mchezo wa leo limewekwa kambaini na Mlinzi Henock Inonga kipindi cha kwanza.

Mpaka sasa Msimamo wa kundi C, Raja Athletic Club wanaongoza wakiwa na alama 6 baada ya michezo miwili, Horoya alama 4 baada ya michezo miwili, Simba wanasogea mpaka nafasi ya tatu wakiwa na alama zao 3 baada ya michezo mitatu na Vipers wanaburuza mkia wakiwa na alama 1 pekee.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live