Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka East Africa Radio, Samwel Rashid mwenyewe anajiita Wakanda Republic amesema kuwa Klabu ya Simba wanapaswa wabadilishew malengo yao badala ya kuishia robo fainali kila mwaka kwenye michuano ya Kimataifa.
Wakanda amesema hayo mara baada ya Simba kuishia kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya African Football League kufuatia kutolewa na Klabu ya Al Ahly ya nchini Misri.
"Simba inatakiwa wabadilishe malengo yao, au kuishia kwenye hizi hatua za robo fainali kwao isiwe mafanikio bali iwe ni fedheha, kwa sababu Standard unai-set kwa namna gani?
"Standard unai-set kwa kufika hatua fulani kwa mfululizo, umeshafika hatua ya makundi kwa mfululizo, umevuka, umeenda hatua ya robo fainali umeshaifika mfululizo, kwahiyo sasa utoke hapo uende sehemu inayofuata ya nusu fainali.
"Kwa sababu kama utaendelea kuishia hatua ya robo fainali ina maana haukui, kwamba wewe umedumaa kwenye hatua moja.
"Kwa sababu kama wewe una mfululizo wa kuishia hatua ya robo fainali, robo fainali, robo fainali ina maana umeishia sehemu kwamba uwezo wako ndio huo umedumaa kwenye hilo eneo," amesema Wakanda Republic.