Simba SC imebadili staili ya kuhamasisha mashabiki wake kuelekea mchezo wao wa Kimataifa dhidi ya Vipers SC utakaochezwa Jumanne ijayo, Marchi 7, 2023 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.
Afisa Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema, Jumapili hii watakuja na hamasa ya Kibichibichi ambapo, mashabiki na wanachama wa Simba, watakutana kwnye fukwe za Coco Beach jijini Dar kula bata na kuhamasishana kuhusu mchezo huo.
"Kispika kinakuja kwa staili nyingine, tutakutana Coco Beach pale tunakula bata tukiwa tumevalia jezi zetu za Simba, tunakula mihongo huku tunapart huku tukihamashishana," alisema Ahmed.
Mbali na hilo, Simba pia wamekuja na staili mpya ya kuuza tiketi maalum za mchezo huo kwa kuwafuata mashabiki wapya kwenye makampuni mbalimbali kisha kuwahamaisha wanunue tiketi maalum zitakazowawezesha wafanyakazi wa makampuni kwenda kushuhudia mechi hiyo.