Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wababe, Kagere hashikiki

75655 Pic+simbazz

Fri, 13 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

SIMBA imeendeleza ubabe baada ya kuibuka na ushindi katika mchezo wao wa pili wa Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar.

Mechi hiyo imechezwa uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ambapo Simba imeibuka na ushindi wa bao 2-1 na kukusanya pointi sita kwa mechi mbili zilizowaweka kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo wakiwa pia na magoli matano ya kufunga na kufungwa mawili.

Kipindi cha kwanza timu zote zilikuwa zinacheza kwa kushambuliana na kila mmoja akionyesha kuhitaji goli la kungoza katika mchezo huo.

Simba ambao walikuwa ndio wenyeji walikuwa wakitumia zaidi kiungo wao Saharaf Shiboub ambaye alikuwa makini kuhakikisha anamiliki mpira na kusambaza kwa ufasaha.

Kwa upande wa Mtibwa Sugar wao walikuwa wanamtumia winga wao, Ismail Aidan ambaye aliionekana kutokuwa na kazi katika kupeleka mashambulizi kwa haraka.

Simba ilipata goli la kwanza kupitia Meddie Kagere dakika 17  baada ya kumalizia krosi ya Mohamed Hussein 'Tshabalala' ambayo iliingia na kwenda kukutana nayo moja kwa moja na kuweka mpira wavuni.

Goli hilo la Kagere linamfanya Kagere kuongoza katika ufungaji baada ya kufikisha magoli matatu ambapo magoli mawili aliyafunga katika mchezo wa kwanza dhidi ya JKT Tanzania.

Dakika 20, Mtibwa Sugar walisawazisha bao hilo kupitia Riphat Khamis, baada ya kuonganisha kwa kichwa kona  iliyopigwa na Ismail Aidan, bao hilo liliwafanya  wachezaji wa Mtibwa kurejea mchezoni.  

Dakika 45 Abdulrahim Humud alipewa kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi Shiboub alipokuwa anamiliki mpira.

Kipindi cha pili, Simba walianza kwa kasi zaidi na kuonyesha dhahili hawajaridhika na matokeo hayo kwani mara kwa mara walikuwa wanafika langoni mwa Mtibwa lakini umakini katika umaliziaji ulikuwa mdogo.

Simba ilifanya mabadiliko dakika 63 kwa kumtoa Hassan Dilunga na kuingia Miraj Athuman, mabadiliko haya yalionyesha dhahili kuhitaji matokeo kutokana na Miraj ni miongoni mwa wachezaji wenye kasi huku Mtibwa Sugar wakimtoa Haruna Chanongo na kuingia Omary Hassan.

Mabadiliko ya Miraj yalijibu baada ya dakika 69 kuifungia goli la pili Simba baada ya kupokea pasi mpenyezo ya Shiboub na kukunjuka shuti kali na kwenda moja kwa moja wavuni huku kipa Shaban Kado akiishiwa la kufanya.

Mashambulizi ya Mtibwa Sugar yalionekana kusimama kutokana na mshambuliaji wao, Riphat kuwa chini ya ulinzi mkali wa Erasto Nyoni na Tairone Santos.

Dakika 79 Simba walifanya mabadiliko mengine ya kumtoa Clatous Chama na kuingia Francis Kahata wakati huo huo Mtibwa Sugar walimtoa Issa Rashid ambaye aliumia na nafasi yake ilichukuliwa na Henry Joseph kwenda kuongeza nguvu eneo la kiungo.

Mtibwa walionekana kuzidiwa zaidi na Simba nafasi ya kiungo kwani Shiboub, Mzamiru Yassin waliweza kutawala na dakika 90 Shiboub alitolewa nafasi yake ilichukuliwa na Jonas Mkude na dakika hiyo hiyo Salum Kanoni alionyeshwa kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi Miraj Athuman.

Chanzo: mwananchi.co.tz