Mchezo wa kwanza hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Arika, unakamilika huku Simba SC wakikubali kichapo cha bao 1-0 ugenini mbele ya Horoya ya Nchini Guinea.
Mchezo huo wa kundi C umepigwa katika Uwanja wa Jenerali Lansana Conte nchini Guinea.
Goli pekee katika mchezo wa leo limefungwa na P.Ndiaye kipindi cha kwanza akiunganisha mpira wa kona dakika ya 18 ya mchezo.
Licha ya kupoteza mchezo huo Simba wametengeneza nafasi nyingi kipindi cha pili lakini ukosefu wa umakini umesababisha kutopata goli.
Mlinda mlango wa Simba, Aishi Manula aliokoa mkwaju wa penati iliyopigwa na Ndiaye kipindi cha pili baada ya Onyango kushika mpira ndani ya eneo la hatari.
Simba wanarudi nyumbani kuja kujiwinda dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco wikiendi ijayo.
Mpaka sasa kundi C linaongozwa na Raja wenye alama tatu, wakifiatiwa na Horoya wenye alama tatu pia, Simaba nafasi ya tatu na Vipers wakiburuza mkia.