Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba waandaliwa dakika 90 za moto

Garrido Kocha mkuu wa Wydad Casablanca, Juan Carlos Garrido

Tue, 25 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha mkuu wa Wydad Casablanca, Juan Carlos Garrido amesema licha ya matokeo waliyoyapata dhidi ya Simba, bado wana mchezo mwingine wa kujitetea wakiwa nyumbani.

Wydad imefungwa 1-0 na Simba bao lililowekwa wavuni na Jean Baleke mchezo uliochezwa juzi Uwanja wa Mkapa.

Akizungumza baada ya mchezo, Garrido alisema walipambana vya kutosha lakini hawakutumia vizuri nafasi walizopata na sasa nguvu wanahamishia mechi inayofuata.

“Tutafanya uchambuzi wa mechi hii ili kuhakikisha kwenye mechi ijayo tunapata matokeo mazuri;

“Tumecheza kipindi cha kwanza hapa ugenini na tunakwenda nyumbani kucheza kipindi cha pili tuna imani tutafuzu hatua inayofuata.”

Garrido amesema watakuwa na hali nzuri kwenye mchezo wa marudiano kuhakikisha wanatumia vizuri nafasi.

“Tulikuwa na nafasi nyingi nzuri za kufunga kwenye kipindi cha kwanza lakini haikuwa hivyo, wenzetu wametumia nafasi waliyopata.

“Hali ya hewa ya kucheza saa 10 jioni sio rafiki sana kwetu japokuwa imechangia kwa kiasi chake lakini isiwe sababu, tunajiandaa kwa ajili ya mchezo ujao.” Wydad na Simba zitarudiana Aprili 28 nchini Morocco.

Chanzo: Mwanaspoti